RASHFORD AULILIA MGUU WA CRISTIANO RONALDO

KINDA wa Manchester United, Marcus Rashford amemtaja straika wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo kuwa ndiye mfano aliopania kuufuata katika kipindi atakachokuwa akikipiga katika klabu hiyo ya Old Trafford.

Zao la timu ya vijana wa Man United lilitamba msimu uliopita kwa kufanikiwa kufunga mabao mawili dhidi ya Midtjylland katika mechi ya Ligi ya Europa iliyopigwa Februari, 25 kabla ya kurudia kufanya hivyo dhidi ya Arsenal katika michuano ya Ligi uu England siku tatu baadae.

Tangu kipindi hicho, Rashford alionekana kuwa tishio katika kikosi cha Man United na baada ya kukosa namba katika kikosi cha kwanza cha Jose Mourinho mwanzoni mwa msimu huu, lakini kwa sasa ana mabao manane katika mechi saba alizocheza katika mashindano yote.

Hata hivyo pamoja na hali hiyo kinda huyo mwenye umri wa miaka 18 amepanga kufuata nyayo za mwanasoka wa zamani wa klabu hiyo ya Old Trafford.

“Kipindi hiki Ronaldo ni mfano wa kuigwa,” nyota huyo aliuambia mtandao wa Sky Sport.


“Unapompanga kwenye safu ya ushambuliaji ni lazima afanye kweli na wapinzani huwa wanamuogopa. Kwa kuwa ni mshambuliaji anayeogopwa, ndicho kitu ambacho nimekipania,” aliongeza staa huyo.

No comments