RAY KIGOS AWATAKA WASANII WA FILAMU KUJITUMA BILA KUTEGEMEA "TAWIRE"

MKONGWE wa filamu hapa nchini, Vincent Kigosi “Ray” amesema kujituma na kuandaa kazi zenye ubora ndio njia pekee itakayosaidia kuifanya Bongo Movies kupata mafanikio ndani na nje ya nchi.

Ray alisema kuwa hakuna njia ya mkato ambayo inaweza kumfanya msanii akapata mafanikio zaidi ya kujituma huku akiwabeza wale wanaoamini ushirikina akisema wanapoteza muda.

“Mimi niliwahi kutuhumiwa kuwa mafanikio yangu yanatokana na ushirikina, lakini ukweli ni kwamba ubora wa kazi zangu ndio ulionifikisha hapa nilipo na wanaotaka mafanikio waige mfano huo,” alisema Ray.

Alieleza kuwa endapo Bongo Movies itachanganywa na ushirikina itakufa haraka na kusababisha wasanii kubaki na njaa na hasa wale ambao bado hawajawekeza.


Ray alisema kama wasanii wenzake watarekodi filamu zenye ubora, anaamini ushindani uliowahi kuwepo kati yake na Steven Kanumba utarejea na watapata mauzo mazuri.

No comments