RAYVANNY: SIO MAPENZI TU, WASANII PIA TUTUNGE KUHUSU CHANGAMOTO ZA KIJAMII

MSANII Raymond “Rayvanny” kutoka WCB amesema kuwa pamoja na kuimba mapenzi, wasanii hawana budi kutunga nyimbo zinazogusa mambo mbalimbali ya kijamii, ikiwemo hali halisi ya maisha ya uswahilini.

“Ukifuatilia wimbo wangu wa “Kwetu” nimezungumzia hali halisi ya maisha ya uswahilini na jinsi vijana wa huko wanavyofanya, ili ikiwezekana wasaidiwe,” alisema.

Rayvanny alisema kuwa uswahilini kuna mambo mengi ambayo yanafanywa na vijana ikiemo uvutaji wa bangi na matukio mengine yasiyofaa, ambayo ni vyema yakazungumziwa ili kupatiwa ufumbuzi.

Msani huyo alisema alichofanya ni kufuata nyayo za bosi wake, Diamond Platnumz ambaye aliibuka na wimbo wa “Mbagala” uliokuwa ukizungumzia maisha halisi ya uswahilini.


Rayvanny anashukuru kuona wimbo wake huo umetazamwa mara mil. 4.3 kwenye Youtube, akisema hilo ni uthibitisho wa jinsi gani alichokiimba kimewagusa wengi. 

No comments