Habari

REAL MADRID, BARCELONA WAPIGANA VIKUMBO KUMWANIA VICTOR LINDELOF

on

KLABU mahasimu katika La Liga,
Real Madrid na Barcelona zimeingia katika vita vya usajili wa msimu ujao na
kujikuta wakimwania kwa pamoja Victor Lindelof.
Pamoja na vigogo hao wa Ligi ya
Hispania, pia Manchester United wanatajwa katika mbio hizo za kumwania nyota
huyo wa klabu ya Benfica.
Mlinzi huyo kijana amekuwa
katika kiwango bora katika msimu huu kiasi cha kuzigonganisha timu mbalimbali,
lakini Sky Sports imezitaja Barca na Real Madrid kuwa ndizo zilizoonyesha nguvu
kubwa kupata saini yake.
Lindelof mwenye umri wa miaka 21,
yumo pia katika kikosi cha timu ya taifa ya Sweden, alikuwa katika orodha ya
wachezaji wanaoweza kuuzwa, lakini tarifa za hivi karibuni zimesema kuwa,
Benfica imesitisha azma hiyo.
Imebainika kuwa, Benfica
imesitisha nia ya kumweka sokoni beki huyo baada ya kuondokewa na mlinzi wao
mahiri, Renato Sanches aliyejiunga na Bayern.
Katika kuhakikisha haimpotezi Lindelof,
imeamua kuweka mezani ofa kubwa ya euro mil 40 ambapo imebainika klabu za Barca
na Madrid wanaweza wasipande dau hilo.

Wakati ambapo Real Madrid
wakishikilia msimamo wa kutaka kumng’oa beki huyo kwa upande wa Barcelona
tayari wameripotiwa kumwania mlinzi atakayeziba nafasi ya Marc Bartra.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *