REMIX YA WIMBO "SALOME" YANUKIA... sauti za Harmonize, Rich Mavoko pia ndani

WAKATI wimbo “Salome” wa Diamond Platnumz ukiendelea kutamba kuna uwezekeano wa kuisikia “remix” ya wimbo huo ambao ndani yake kutakuwa na sauti ya Harmonize na Rich Mavoko.

Hayo ni maneno ya Harmonize aliyoandika kwenye mtandao wake wa Instagram akisema “Unatamani kusikia sauti yangu na Rich Mavoko kwenye "Salome remix,” aliuliza Harmonize na kuweka picha kwenye mtandao huo ikiwaonyesha wakiwa Studio.

Naye Rich Mavoko hakutaka kupitwa na hilo, alijazia kwa kuandika kwenye picha aliyoiweka kwenye mtandao huo kuwa: “Eti unatamani kusikia sauti yetu ya pamoja.”


Wimbo huo uliimbwa na Saida Karoli mwanzoni mwa mwaka 2000 lakini sasa Diamond aliamua kuurudia akiwa amemshirikisha Raymond na ameonekana kufanya vizuri kwenye kila kona huku ukitazamwa zaidi kwenye mtandao wa You tube.

No comments