RIYAD MAHREZ AKIRI KUWINDWA NA ARSENAL

STRAIKA wa Leicester City, Riyad Mahrez ameweka wazi kuwa Arsenal walijaribu kumsajili mwishoni mwa msimu uliopita lakini Leicester City walizuia mpango huo.

Mahrez aliongeza kuwa mabingwa hao watetezi hawakutaka kumwachia na hakuona sababu ya kulazimisha uhusiano huo na ndio maana alibaki kwenye kikosi hicho cha Claudio Ranieri.


“Kulikuwa na mawasiliano na Arsenal lakini Leicester bado walikuwa ghali sana, kwa upande wangu naona ni wazo nzuri kubaki hapa,” alisema.

No comments