RIYAMA ALLY AJIFAGILIA MWENYEWE KUHUSU KUZITENDEA HAKI FILAMU ZA KIBONGO

MSANII machachari wa filamu, Riyama Ally amesema kuwa anajua kuitendea haki Bongomuvi ndio maana amekuwa na jina kubwa kwa vile anaigiza kwa kufuata muswada na maelekezo ya waongozaji wa filamu.

“Hiyo ndio siri kubwa ambayo inanifanya nipendwe na watu wengi, kwasababu ninazingatia na kuuvaa uhalisia kama inavyotakiwa kufuata maelekezo ya waongozaji wa filamu,” alisema.

Msanii huyo alisema huwa anabadilika kulingana na ujumbe wa filamu husika na hataki kufanyakazi itakayokuja kukataliwa sokoni, ndio maana anajitahidi kuzitendea haki filamu zote na kujizolea sifa tele kutoka kwa mashabiki ambao wamempachika jina la “malkia wa uswazi.”


Alisema kuwa jina hilo linatokana na jinsi anavyotumia vizuri misemo ya uswahilini katika filamu na kuwa kivutio kikubwa kwa wale wanaofatilia Bongomuvi.

No comments