ROMELU LUKAKU AMFAGILIA KOCHA THIERRY HENRY

STRAIKA wa Ubelgiji, Romelu Lukaku amekubali uwezo wa kocha msaidizi wa timu ya taifa ya nchi hiyo, Thierry Henry na kuongeza kuwa ana mengi ya kujifunza kutoka kwa mkongwe huyo wa Arsenal.

Lukaku alikuwa mmoja kati ya wachezaji waliotikisa nyavu katika mechi ya ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Bosnia-Herzegovinaa katika mechi ya kusaka tiketi ya kwenda kucheza Kombe la Dunia 2018.

“Nadhani (Henry) ananifundisha mambo mengi, anazungumza kwa uwazi kwangu," alisema Lukaku wakati akiteta na waandishi wa habari baada ya mechi kumalizika.

“Najua nini kizuri napaswa kufanya na inapotokea nafanya tofauti na maelekezo yake hasiti kuniambia. Nafurahi msahada wake kwangu."


“Anatusaidia washambuliaji na timu, kiujumla amejenga uwezo wa wachezaji kucheza kitimu uwanjani," alisema Lukaku.

No comments