RONALDO APIGWA TOBO MAZOEZINI NA KUWANUNIA WACHEZAJI WENZAKE

KUNA mambo mengine yanayofanywa na mastaa unaweza kushangaa. Sikia hii. Winga wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo alijikuta akijawa na hasira baada ya kupigwa tobo wakati wa mazoezi ya timu hiyo.

Staa huyo alikuwa akifanya mazoezi ya kugombea mpira na wenzake, yaani mchezaji mmoja kuwa katikati ya wengine na kuutafuta mpira, ndipo alipopigwa tobo (mpira kupita katikati ya miguu yake).

Kilichomkasirisha Mreno huyo ni baada ya mwenzake, Marcelo kufurahia aibu hiyo na kuwapongeza wenzake waliomwaga kicheko cha dharau.

“Sasa mmepata cha kuandika baadae?” alisema Ronaldo kwa hasira, kwa mujibu wa AS.

Haikuishia hapo, Ronaldo, 31, aliamua kuubutua mpira kwa hasira kuelekea sehemu walipokuwa aandishi wa habari.


Kikosi cha Zinedine Zidane kilikuwa kwenye mazoezi kuelekea ratiba ya mwisho wa wiki hii dhidi ya Real Betis.

No comments