RONALDO AWEKA HADHARANI GARI LAKE JIPYA LA KIFAHARI

STRAIKA Cristiano Ronaldo ameonyesha gari lake jipya la kifahari aina ya Lamborghini Aventador lenye thamani ya pauni mil 260, 040.

Habari kutoka nchini Hispania, staa huyo alionyesha mkoko huo Jumatatu baada ya Real Madrid kuibuka na ushindi wa mabao 6-1 dhidi ya Real Betis katika michuano ya Ligi Kuu ya michuano ya La Liga.

Taarifa hizo zinaeleza baada ya kupata ushindi huo Jumamosi usiku, staa huyo alichukua mtandao wake wa Instagram na kutupia picha hiyo akiwa amesimama mbele ya gari hilo la kifahari aina hiyo ya Lamborghini huku ikiwa imeambatana na salamu ya asubuhi njema.

Jumamosi Ronaldo na wenzake walimaza ukame wa kucheza mechi nne bila kushinda kwa ushindi huo mnono dhidi ya Real Betis.


Mabao mawili yaliyofungwa na Isco na moja kutoka kwa Raphael Varane, Karimu Benzema, Marcelo na Ronaldo ndiyo yaliyoifamnya Real Madrid kupunguza pengo dhidi ya mahasimu wao Atletico Madrid kwenye msimamo wa Ligi.

No comments