ROONEY AKIRI KUANZA MSIMU KWA KIWANGO KIBOVU MANCHESTER UNITED

WAYNE Rooney wa Manchester amebainisha ukweli kuwa ameanza msimu kwa kiwango kisichowalidhisha wadau na mashabiki wa klabu yake.

Lakini pamoja na kukiri hilo Rooney amesema amepambana kwa ajili ya kurudisha kiwango chake na kuisaidia timu kupata mafanikio msimu huu.

“Nimeanza msimu katika mwendo usiowaridhishha wengi lakini ninapambana.”

“Nitahakikisha katika muda mchache ujao nitarudi katika kile kiwango ambacho wengi wanakitaka hivyo ni suala la kuendelea kuvumilia tu,” alisisitiza Rooney.

Nahodha huyo wa United ambaye juzi ametimiza miaka 31 aliyazungumza haya muda mchache baada ya kumalizika kwa mechi ya Ligi ndogo ya Ulaya dhidi ya Fenerbahce.

Rooney ambaye kwa sasa akiwa na Man United amechezea mechi 4 akitokea benchi, amesisitiza kuwa yeye yupo tayari wakati wowote akiitwa kucheza.

No comments