ROONEY ASEMA NI AIBU KUBWA KWA BIG SAM KUJIUZULU KUINOA ENGLAND NDANI YA SIKU 67 TU

NAHODHA wa timu ya Uingereza Wayne Rooney amesema moja kati ya aibu ambazo amewahi kushuhudia ni kijiudhuru kwa kocha wa timu ya Taifa hilo, Sam Allyardyce maarufu kama “Big Sam.”

Akiongea na BBC Sport, Wayne amesema kwamba hana mashaka kwamba kocha huyo ni moja ya watu maarufu na muhimu lakini hatua yake ya kubwaga manyanga katika timu ya taifa ni jambo la aibu.

Rooney amesema hatua hiyo ya kuacha kazi baada ya siku 67 tu ni jambo la aibu ambalo amesema haliwezi kuisafisha England katika wakati mfupi tu.

“Hii ni aibu, huwezi kusema kwamba tumeshawahi kupata aibu nyingine kama hii katika soka,” amesema Rooney.

“Big Sam ni kocha mzuri sana. Sijui nini kimetokea lakini pia sijui nani anawajibika moja kwa moja katika aibu hii,” amesema.


Lakini Rooney amesema anajua kwamba Uingereza ni nchi kubwa ambayo inaweza kumpata kocha mbadala wa Big Sam katika mazingira yoyote yale. 

No comments