RUBY ASEMA WIMBO WAKE WA "WALEWALE" SIO DONGO KWA YEYOTE

NYOTA wa Bongofleva, Irene George “Ruby” ambaye sasa anatamba na wimbo wa “Walewale”, amefunguka na kusema kuwa wimbo huo sio dongo kwa mtu bali amemwimba shetani.

Ruby alisema kuwa wimbo huo una ujumbe ambao utawafanya watu kujitambua na kujiondoa katika vifungo vya shetani ambavyo vinawasumbua katika maisha yao.

“Sijaimba huu wimbo kwa ajili ya mtu kama ambavyo baadhi wanavyofikiri na sijaimba mapenzi kabisa humu ndani kama ambavyo watu wanavyomuongelea Ruby kuwa anaimba mapenzi tu. Nimemwongelea shetani na sifa zake,” alisema Ruby.

Alisema shetani so mtu na wala hajafanana na binadamu ila ni roho ambayo inaweza ikamwingia mtu yeyote.

“Hiyo roho inaweza ikakuletea kitu kizuri na kumbe inataka ikutawale halafu ikuharibie, lakini kitu kizuri na cha kudumu ni cha Mungu.”


“Hivyo vitu hutokea kwa mabosi wetu, pengine bosi akakutaka kimapenzi ili akupandishe cheo, lakini ile hali sio hali nzuri, kwahiyo mimi sijamuongelea mtu yeyote bali ni shetani ambaye mara nyingi anataka kutuharibia maisha yetu,” alisema.

No comments