RYAN GIGGS AKIRI KUMWONEA HURUMA WAYNE ROONEY

GWIJI wa zamani wa Manchester, Ryan Giggs amekiri kuwa anbamuonea huruma nahodha wa Manchester United, Wayne Rooney ambaye anahaha kupata namba kikosi cha kwanza kwa klabu na timu ya taifa.

Mchezaji huyo, 30, alianzishwa benchi na meneja wa muda wa Uingereza Gareth Southgate Jumanne usiku katika sare ya 0-0 dhidi ya Slovenia.

Rooney pia amekuwa miongoni mwa wachezaji wa akiba katika kikosi cha Manchester United mechi tatu chini ya Jose Mourinho.

“Namwonea huruma,” Giggs aliiambia ITV. “Kuelekea mwishoni mwa msimu uliopita na kwa Uingereza majira ya joto alichezeshwa kama kiungo kisha akaambiwa atacheza kama namba 9 au 10. Kwa kiasi fulani alichanganyikiwa.”

“Namna pekee ya kumrejesha kwenye kiwango ni mazoezi. Simuoni akicheza kwenye namba moja, anakipaji cha kucheza kwenye nafasi tofauti na uzoefu mkubwa.”


Rooney anatumaini kurejea kwenye ikosi cha Manchester United Jumatatu usiku dhidi ya Liverpool katika uwanja wa Anfield.

No comments