SADIO MANE ALIZIMIKIA TABASAMU LA RONALDONHO

Liverpool's summer arrival Sadio Mane looks focused in training on Wednesday

STAA wa Liverpool Sadio Mane ametoboa kuwa alivutiwa na uchezaji wa aliyekuwa staa wa klabu ya Barcelona na timu ya Taifa ya Brazil, Ronaldinho lakini alipenda zaidi tabasamu lake.

Mane ambaye ni raia wa Senegal aliyejiunga na Liverpool akitokea Southampton kwa ada ya uamisho wa pauni mil 34, amesema kuwa amekuwa akiiga tabasamu la mkongwe huyo kila anapokuwa uwanjani.

“Mara nyingi Ronaldinho alifanya hivyo na najitahidi kufanana nae nafikiri soka lina mengi ya kufanya utabasamu. Tunafanya kazi kubwa ambayo kila mmoja alipanga kuwa nayo,” alisema Mane.

Mashabiki wa Arsenal watakuwa na furaha baada kuambiwa kwamba mchezaji wao Hector Bellerin, aliyedaiwa kupata majeraha ya kifundo cha mguu amefanya mazoezi na kikosi cha vijana cha Hispania chini ya umri miaka 21.


Katika mchezo wa timu ya taifa ya Hispania ya vijana chini ya umri wa miaka 21 dhidi ya San Marino iliochezwa katikati mwa wiki iliyopita, Bellerin alichezewa vibaya baada ya kudaiwa kuumia kifundo cha mguu wa kulia lakini juzi alidaiwa kufanya mazoezi na wenzake na yupo vizuri kwa sasa.

No comments