Habari

SADIO MANE ASEMA ALIITOSA MANCHESTER UNITED NA SASA ANAKWENDA KUWATUNGUA AKIWA NA LIVERPOOL

on

SADIO MANE amesisitiza kuwa ni yeye aliyeamua kubakia Southamtpon mwaka 2015 licha ya Manchester United kuweka mezani pauni milioni 25.
Mshambuliaji huyo alikuwa lengo kuu la kocha Louis van Gaal na ilidhaniwa kuwa ni Southampton ndiyo waliokataa kufanya biashara, lakini sasa wakati akielekea kucheza ‘derby’ ya kwanza ya United na Liverpool, nyota huyo wa kimataifa wa Senegal anaweka wazi kuwa ni yeye aliyeamua kuitosa Manchester United.
Mane mwenye umri wa miaka 24, amekuwa kwenye kiwango cha kutisha tangu asajiliwe na Liverpool kiangazi hiki chini ya kocha Jurgen Klopp ambapo ameshatupia wavuni mabao matatu katika mechi sita za Premier League alizocheza.
Akizungumza na gazeti la The Telegraph la Uingereza, Mane aliyetua  Liverpool kwa pauni milioni 30 alisema:”Hakika kulikuwa na klabu kadhaa zilizonitaka lakini sikuchagua hata moja, nilitaka kubakia Southampton.
“Kocha Ronald Koeman alichukizwa na uvumi wa usajili wangu kwasababu alitaka nibakie. Hilo halikuwa jambo gumu kwasababu mimi mwenyewe pia sikutaka kuondoka.
“Nilipokutana na Koeman nikamwambia asitie shaka, nitabakia. Ulikuwa ni uamuzi wangu, nilitaka kubakia Southapmton nikiamini kuwa bado kuna vitu natakiwa kufanya hapo ili kuthibitisha ubora wangu.
“Ni hadi Liverpool walipokuja mwaka mmoja baadae ndipo nilipoona kuwa sasa ni wakati muafaka wa kuondoka, sikutaka kufikiria mara mbili.”
Jumatatu usiku Liverpool itaikaribisha Manchester United iliyosukwa upya chini ya Jose Mourinho ambapo Mane amesema ana furaha kubwa kucheza dhidi ya United.
“Tunakwenda kuwafunga Manchester United. Hakika hatuna wasiwasi, kila mchezaji anajiamini kuwa ushindi utapatikana,” alisema Mane.
 Mane (second left) jumps on Jurgen Klopp's back after his goal against Arsenal on August 14

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *