SADIO MANE ASEMA ANAJIVUNIA KUMEZEWA MATE NA MANCHESTER UNITED

STAA wa Liverpool Sadio Mane amesema kitendo cha kumezewa mate na Manchester United mwaka mmoja uliopita kilimfanya ajijengee kujiamini katika kipindi cha misimu michache iliyopita.

Mane anatajwa kuwa kati ya wachezaji tishio katika michuano ya Ligi Kuu na Man United inasemekana kummezea mate msimu uliopita.

“Kwa kuwa muwazi kuna klabu nyingi ambazo zilikuwa zikimfuatilia kipindi hicho lakini sikuzipenda,” alisema staa huyo.


“Sikufanya mazungumzo na klabu yoyote kwa sababu nilikuwa nikitaka kucheza mahali hapa,” aliongeza staa huyto.

No comments