SERGE AURIER KUTUPWA JELA MIEZI MIWILI... kisa ni kufanya vurugu mbele ya kituo cha polisi

MLINZI wa Paris Saint-Germain, Serge Aurier anaweza kutumikia kifungo cha miezi miwili jela baada ya kufanya vurugu mbele ya kituo cha polisi.

Vyanzo mbalimbali nchini Ufaransa vilisema licha ya kupangiwa kifungo hicho, lakini anaweza kufanya kazi za jamii kwa miezi miwili.

Pia nyota huyo wa Ivory Coast amepigwa faini ya pauni 520. Hadi sasa vyanzo vya ndani vinasema Aurier amethibitisha kuwa yuko mbioni kukata rufaa na kuna uwezekano wa kuonekana katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya katikati ya juma hili dhidi ya Ludogorets.


Ikumbukwe anaonekana kurudia makosa aliyoyafanya Mei, mwaka huu katika Paris Night Club alipowakaripia maofisa wa polisi.

No comments