SHAMSA FORD ADAI MAISHA YA NDOA KWAKE RAHA TUPU

MWANADADA mrembo wa filamu za Bongo, Shamsa Ford amekiri kupata raha ndani ya ndoa kwa sasa kwani amejikuta ana furaha isiyo na kifani.

Mwigizaji huyo miezi miwili iliyopita alifunga ndoa na mfanya biashara wa maduka ya nguo, Chidi Mapenzi.

Shamsa amesema ndoa imempatia amani ya moyo ambayo alikuwa anaitafuta kwa muda mrefu.

“Nashukuru Mungu kwa afya njema na kwa kila kitu kikubwa, ndoa imebadilisha vitu vingi sana katika maisha yangu,” alisema Shamsa.


“Kwanza imenifanya niache baadhi ya vitu na kuongeza badhi ya vitu katika maisha yangu,” aliongeza msanii huyo.

No comments