SHAMSA FORD ASEMA NI ZAMU YAKE “KUOKOKA”

MSANII wa filamu nchini, Shamsa Ford amebainisha wazi kuwa anataka kubadilisha mfumo wa maisha yake kwa kufanya ibada na kumtumikia Mungu pamoja na kuishi kwa matendo ya kumpendeza Mungu.

Hali hii imeibuka mara baada ya msanii huyo kufunga ndoa na mfanyabiashara maarufu jijini Dar es Salam, Chidi Mapenzi.

Mwigizaji huyo ametangaza uamuzi huo ikiwa ni miezi michache toka afunge ndoa na mfanyabiadshara huyo wa maduka ya nguo.

“Maisha ya kuendekeza dunia nimeyachoka. Natamani ifike siku kwa kudra za Mwenyezi Mungu nibadilike. Natamani niwe mmoja wa wale watakaopata nafasi ya kwenda popote pamoja na familia yangu.”


Mashabiki wa Shamsa katika mitandao ya kijamii wameonyesha kupendezwa na uamuzi huo, huku wachache wakimuuliza maswali kama ataendelea kufanya tena filamu.

No comments