SHARAPOVA APUNGUZIWA ADHABU YA KIFUNGO... sasa kutumikia miezi 15 badala ya miaka miwili

CHAMA cha tenesi duniani (ATF), kimempunguzia mchezaji nyota wa tenesi Maria Sharapova adhabu ya kifungo cha miaka miwili na sasa itakuwa miezi kumi na tano lakini kimesema kuwa wachezaji wa mchezo huu hawataruhusiwa kukata rufaa kama watahusishwa kuhusika kwa makusudi na matumizi ya dawa zilizokataliwa michezoni.

Katika taarifa yake, chama hicho kimesema kuwa hakitakuwa tayari kupokea maelezo yoyote ambayo yanaonyesha kuwa mchezaji alitumia dawa hizo kwa makusudi baada ya taarifa zote kiutolewa.

Sharapova ni mshindi mara tano wa Grand Slam na kwa mujibu wa jarida la Forbes ni mwanadada anayelipwa zaidi katika mchezo huo kwa miaka 11 mfululizo mpaka alipopitwa na Serena Williams mwaka huu.


Sharapova aligundulika kutumia dawa hizo karibia mwezi mmoja tokea zilipofungiwa Januari 2016.

No comments