SHILOLE ADAI WIMBO WAKE WA "MTOTO MDOGO" UNATETEA "SERENGETI BOY" KWENYE JAMII

MKALI wa kike wa Bongofleva, Zuwena Mohammed “Shilole” amesema kuwa wimbo wake wa “Mtoto Mdogo” una ujumbe maalum kwa ajili ya kuikumbusha jamii kwamba mapenzi ya sasa hayajali umri.

“Binafsi kwa muda mrefu nimekuwa nikisemwa sana kwamba nina uhusiano wa kimapenzi na watoto wadogo, lakini kiukweli kwa sasa mapenzi hayajali umri ilimradi kukubaliana tu,” alisema.

Shilole alisema ameona afikishe ujumbe wake kwa njia ya wimbo kwa wale ambao wamekuwa wakimfuatilia maisha yake na kumuona kanakwamba hafai kwenye jamii.


Amesema haoni kosa wala ubaya wowote kijana wa kiume kupendana na mwanamke mwenye umri mkubwa ama mtu mzima kumpenda msichana mdogo, ilimradi tu awe amefikisha umri wa miaka 18, kwa vile ndio mapenzi yalivyo.

No comments