SHILOLE AJISIFU ANA MOYO WA KUPENDA MAFANIKIO YA WASANII WENZAKE

NYOTA wa muziki wa Kizazi Kipya asiyeishiwa vituko, Zuwena Mohammed “Shilole” amesema ana moyo wa kupenda mafanikio ya wasanii wenzake ndio maana huwa hana maringo pale wanapohitaji kushirikiana naye.

Shilole alisema kuwa kukubali kuwa “Video Queen” kwenye wimbo wa Man Fongo na wa Rayvanny ni dalili kwamba ana moyo wa kupenda kusaidia wasanii wenzake ili nao wapate mafanikio.

“Ninasema hivyo kwa sababu hakuna siri kuwa hapa Tanzania kuna wasanii wanaojiona wapo matawi ya juu, hawako tayari kushirikishwa kwenye nyimbo za wasanii wanaochipukia,” alisema Shilole.

Msanii huyo aliongeza kuwa anatambua utafika wakati umri “utamtupa mkono” na hatakuwa na uwezo wa kupanda jukwani, hivyo ni muhimu asaidie wasanii wanaochipukia ili nao watimize ndoto zao.


“Muziki hauhitaji hasira wala kuoneana wivu, tunatakiwa kushirikiana bila kubaguana,” alisema.

No comments