SIKINDE KUMIMINA UHONDO MANGO GARDEN KINONDONI IJUMAA HII


WAKALI wa muziki wa dansi hapa nchini Mlimani Park “Sikinde Ngoma ya Ukae”, Ijumaa hii wataangusha burudani nzito ndani ya ukumbi wa Mango Garden Kinondoni.

Mara ya mwisho Sikinde kutumbuiza Mango Garden, ilikuwa ni  mwezi Machi mwaka huu wakati waliposindikiza uzinduzi wa bendi ya Double M Plus.

Mratibu wa onyesho hilo, Juma Mbizo ameiambia Saluti5 kuwa kutakuwa na ‘surprise’ ya wasanii nyota ambao nao watapata fursa ya kulisabahi jukwaa la Sikinde.

No comments