SOGGY DOGGY HUNTER ASOMA SOKO LA MUZIKI ILI KUANZA KUTOKA TENA

RAPA aliyewahi kutamba vilivyo, Soggy Dogg Hunter ameshafikisha nyimbo 16 ambazo tayari ameshazirekodi lakini hajaanza kutoa kwa madai kwamba anasoma soko la muziki.

“Kwanza kabisa ni kwamba sijaacha muziki licha ya kwamba sijasikika nikitoa kazi mpya kwa kipindi kirefu, hapa nilipo nina kama ngoma 16 hivi zipo tu utazisikia muda si mrefu kwani bado nina soma mchezo,” alisema. 

Alisema kuwa wakati baadhi ya wasanii wenzake wakibadilika katika muziki yeye anaendelea na mtindo uleule kwa kuwa ni mwana Hiphop.


Soggy alisema kuwa hawezi kuimba wala kufanya singeli hivyo ataendelea na Hiphop kama kawaida kwa vile ndio uliofanya akajulikana kwa mashabiki akiwa na nyimbo mbalimbali ukiwemo wa “Kibanda cha 
Simiu”.

No comments