STEVE NYERERE APOTEZEA KIPIGO CHA BONGOFLEVA CHA MABAO 5-4 DHIDI YAO

MSANII wa vichekesho, Steve Nyerere amesema kuwa licha ya timu ya Bongomuvi kula kichapo katika mechi dhidi ya timu ya Bongofleva, lengo la kuchangia waathirika wa tetemeko mkoani Kagera limetimia.

Alisema, timu ya Bongofleva iliibuka na ushindi wa penati 5-4 dhidi yao katika mechi ya hisani kwa aili ya kuwachangia waathirika hao, hivyo hilo ndilo la muhimu badala ya kutambia ushindi tu.

“Hicho ndicho ninachoweza kusema, kwamba tulicheza mechi ya hisani kwa ajili ya kuwachangia waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera, hilo ndilo lilikuwa lengo kubwa zaidi ya kushindana,” alisema Steve.


Alisema, wapo watu wanachonga kwamba timu ya Bongomuvi ilichapwa na wanasahau kile kilichosababisha hadi mechi hiyo ikaandaliwa na hatimaye kufanyika.

No comments