SWANSEA YAMPIGIA MAHESABU GIGGS KUCHUKUA MIKOBA YA FRANCESCO GUIDOLIN

KLABU ya Swansea City imetupia macho yake kutaka saini ya kocha asie na uzoefu, Ryan Giggs kuchukua nafasi ya Muitaliano Francesco Guidolin (60), endapo wataamua kumfungashia virago.

Imefahamika kuwa mwenyekiti wa klabu hiyo, Huw Jenkins anatamani kumwondoa haraka Guidolin na kumweka mchezaji huyo mkongwe wa zamani wa Manchester United.

Guidolin ambaye ana miezi minne tangu atue katika Ligi Kuu ya England (EPL), anaendelea kujitahidi kukilinda kibarua chake licha ya kupatamkataba wa miaka minne.

Hata hivyo mechi mbili dhidi ya Manchester City na Liverpool zinaonekana kuwa kipimo cha kocha huyo kuendelea kubakia klabuni hapo au la.

Swansea imeanza vibaya msimu huu kwani katika mechi tano za kwanza imeweka kibindoni pointi nne tu.


Hata hivyo swala la kumtimua Guidolin linaweza lisipate nafasi kwa miliki kutoka Marekani Steve Kaplan na joson Levien kutaka kumpa muda zaidi kocha huyo.

No comments