TERRY AMKINGIA KIFUA ROONEY KUHUSU KUPOROMOKA KIWANGO CHAKE CHA UCHEZAJI

WADAU wa soka wa nchini England wanamwangalia jicho baya Wayne Rooney kwa madai kuwa kiungo chake kinazidi kuporomoka.

Lakini beki mkongwe nchini humo, John Terry anapingana na mtazamo huo kwa kusema, Rooney atabakia kuwa nyota muhimu katika soka la England hususan ndani ya kikosi cha timu ya taifa.

Terry alisema hayo wakati akishuhudia England ikiibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya timu ya taifa ya Malta.

Akizungumza Terry alisema huwezi kuwataja wachezaji wa timu ya taifa ya England na ukamweka kando Rooney kwani atakaebakia kuwa mfungaji bora.

“Unapomzungumzia Rooney hupaswi kumwangalia katika mechi za klabu ama Primer pekee bali lazima uangalie mchango wake katika kikosi cha taifa.”

“Mimi simtazami katika ngazi ya klabu bali tunapaswa kumwangalia katika kiwango cha ndani na nje ya Ligi ndipo utakapoona umuhimu wa Rooney.


“Tunamwangalia katika ngazi za msaada kwa timu ya taifa kwa sababu amekuwa mfungaji wa miaka yote, ni vyema tukampa heshima yake.”

No comments