TETEMEKO LA ARDHI KAGERA LAMWIBUA UPYA SAIDA KAROLI

TETEMEKO la ardhi lililotokea hivi karibuni mkoa Kagera limemwibua msanii wa siku nyingi wa nyimbo za asili, Saida Karoli ambaye sasa amekuja na wimbo unaohusu tetemeko hilo.

Saida alisikika kwa kinywa chake akisema kuwa amekamilisha wimbo huo ingawa hakutaja jina lake na kufafanua kuwa maafa yaliyosababishwa na tetemeko hilo ni makubwa hivyo hana budi kutungia wimbo tukio hilo.

Msanii huyo aligusia hilo alipokuwa akizungumzia hatua ya Diamond platnumz kuachia wimbo wa “Salome” ambao yeye (Saida) aliwahi kuuimba mwanzoni mwa mwaka 2000 na kumfanya awe matawi ya juu.


Saida alisema kuwa amefarijika na kujihisi kuzaliwa upya baada ya kuona wimbo wake wa “Maria Salome” ukirudiwa upya na supastaa wa sasa wa Bongofleva, Diamond Platnumz.

No comments