THEA AIOMBA JAMII ISIMPE KILA MSANII WA BONGO MUVI SIFA YA UHUNI

MWIGIZAJI wa siku nyingi wa filamu nchini, Ndumbagwe Misayo “Thea” ameiomba jamii isiwaone wasanii wote wa Bongomuvi ni wahuni kwa sababu tu ya wachache wenye tabia hiyo.

Alisema kuwa ni kweli ndani ya Bongomuvi wapo baadhi ya wasanii ambao wamekuwa wakiifanya fani hiyo ionekane ni ya kihuni na kumbe kuna watu wana heshima zao.

Thea alisema kuwa Bongomuvi ni sawa na kazi nyingine za ofisini na kwamba hata huko nako wapo baadhi ya watu ambao huharibu kazi kwa kufanya mambo yasiyofaa na wanapaswa kukemewa.


“Maana yangu ni kwamba watu wachache wasiifanye Bongomuvi ionekane ni ya wahuni bali hao wanaoichafua wakemewe ili waache tabia hiyo na kurudi kwenye mstari,” alisema.

No comments