THIBAUT COURITOUS ACHEKELEA "LAIFU" LA STANFORD BRIDGE

MLINDA mlango wa Chelsea Thibaut Couritous amesema kuwa anafurahia maisha kwenye klabu hiyo ya Stanford Bridge licha ya kusema kuwa kuna siku moja atarejea nchini Hispania.

Mbelgiji huyo aliwahi kutwaa ubingwa wa La Liga mwaka 2004 akiwa na Atletico Madrid na msimu huu alikuwa akitajwa kwamba angerejea Real Madrid.

Akiwa mara kadhaa ameshatangaza nia ya kurejea nchini Hispania, laini Courtois alisema juzi kuwa bado ana jukumu la kuitumikia Chelsea na akasema kuwa pengine atabaki na timu hiyo hadi atakapostaafu kucheza soka.

“Ninachokifahamu ni kwamba sina matatizo na mashabiki wa Chelsea,” alisema katika mahojiano na gazeti la Mirror.

“Sio kwamba kwa sasa nataka kurejea nchini Hispania, laini naweza kufanya hivyo bada ya kustaafu soka,” aliongeza nyota huyo.


Alisema kwamba kwa sasa anafurahia kuwa sehemu ya Chelsea na kwamba anachokitaka ni kutwaa taji akiwa na klabu hiyo.

No comments