TID ASEMA MUDA WAKE WA KUFANYA KOLABO NA MAN FONGO NI MWAKA 2020

MKONGWE wa muziki wa kizazi kipya, Khalid Mohammed “TID” amesema haezi kufanya kazi na msanii wa muziki wa Singeli, Man Fongo labda hadi mwaka 2020.

TID alisema kuwa sasa ana mambo mengi ya kufanya hivyo hataweza kutenga muda wa kuandaa kolabo na nyota huyo hadi baada ya miaka mine ijayo ndipo anaweza kuwa na nafasi ya kutosha.

“Nitakuwa tayari mwaka 2020 na sio sasa pamoja na kwamba utakuwa mwaka wa uchaguzi lakini ndio kitakuwa kipindi kizuri cha kufanya hivyo, lakini kwa sasa hivi sipo tayari nina kazi nyingi ninazifanya,” alisema TID.


Msanii huyo alisema kuwa kwa muda mrefu mashabiki wamekuwa wakimuomba kufanya kolabo na Man Fongo na sasa ameamua kutoa ufafanuzi ili asionekane kama anajisikia na kumbe amebanwa na muda.

No comments