TIMUATIMUA KUWAKUMBA WACHEZAJI "MIZIGO" CHELSEA

MMILIKI wa Chelsea, Roman Abramovich inasemekana amekerwa na mwenendo wa timu hiyo wa msimu huu wa Ligi na sasa anataka kuuzwa wachezaji wengi na kusajiliwa chipukizi.

Abramovich kwa mara ya kwanza tangu anunue timu hiyo ya Stanford Bridge msimu huu anashuhudia timu yake ikiishia kuwa mtazamaji wa michuano ya Ulaya.

Hilo linamwumiza lakini anaumia anapoona mwanzo unaotia shaka, timu imecheza mechi sita imeshinda tatu kwa mbinde, sare moja na kushindwa miwili, haijaonyesha soka la kuvutia.

Kutokana na hilo, bilionea huyo amemwagiza kocha Antonio Conte aangalie namna ya kuwapiga bei wachezaji wasio na faida tena ili fedha za mauzo na fungu loingine atakalopewa atumie kwa usajili.

Kocha huyo, Conte ameanza katika hali ya kusuasua kama ilivyo kwa mtangulizi wake, Jose Mourinho msimu uliopita.

Mmoja wa watu wa benchi la ufundi amethibitisha kuwa Conte ndie anayepunguza presha ya bilionea huyo akimtaka awe na subira kidogo wasubiri kuona vijana wake watafanya nini katika miezi hii mitatu kabla ya usajili wa mwezi Januari.

Chelsea ilitumia pauni mil 115 kuwasajili wachezaji wanane kiangazi hiki, N’Golo Kante, Michy Batshuayi, David Luiz na Marcos Alonso, lakini hawajaisaidia timu kupata ushindi uliotarajiwa.

Vipigo kutoka kwa Liverpool na Chelsea ndivyo vilivyomtisha Abramovich ambaye amemwambia Conte aache baadhi ya wachezaji ili kusajili walinzi wapya wa kati kusaidiana na nahodha John Terry ambaye anaandamwa na majeruhi lakini pia kiungo na mshambuliaji mwingine mwenye uwezo wa kufunga kumsaidia, Diego Costa.

Safu ya ulinzi imetibuka tangu kuumia kwa Terry, Gary Cahill na Luiz wameshindwa kuelewana huku Cesar Azpilicueta nae akishindwa kufanya vyema katika ulinzi wa pembeni kulia alikohamishiwa baada ya kiwango cha Branislav Ivanovic kuwa chini mno msimu huu.

Hofu ya kuondoka ipo kwa mlinzi maarufu, Ivanovic aliyeshindwa kurejesha kiwango sawa na kiungo Cesc Fabregas, wote wawili mikataba yao itamalizika mwishoni mwa msimu huu.

Wachezaji wanaowimndwa kwa sasa na Chelsea ni mshambuliaji wa Atletico Madrid, Antoine Greizmann pamoja na Alvaro Morata na Romelu Lukaku ambao Conte alijaribu kuwasajili kiangazi hiki bila mafanikio.


Aidha, mlinzi chipukizi wa AS Roma ya Italia, Antonio Rudiger mwenye miaka 23 amekuwa kwenye rada za Conte anayepigania kuimarisha safu ya ulinzi.

No comments