TWANGA PEPETA KUPEPETANA NA MSONDO OKTOBA 30 NDANI YA NEW BULYAGA


Baba ya Muziki - Msondo Ngoma Music Band wataikaribisha Twanga Pepeta kwenye kiwanja chao cha kila Jumapili, New Bulyaga Bar katika onyesho kabambe la funga mwezi.

Onyesho hilo litakalo wakutanisha wababe hao wa muziki wa dansi, litafayika Jumapili ya tarehe 30 mwezi huu ndani ya ukumbi huo wa Bulyaga ulioko Temeke jijini Dar es Salaam.

Muddy K anayeratibu onyesho hilo la kukata na shoka, ameiambia Saluti5 kuwa burudani itaanza rasmi saa 1 usiku ambapo tofauti na Jumapili zingine ambazo kiingilio huwa ni bure, safari hii mashabiki watalizimika kulipa sh. 6000 ili kuzishuhudia Msondo na Twanga Pepeta.

No comments