UMESIKIA HII? SAIDA KAROLI SASA HATAKI TENA KUIMBA NYIMBO ZA KIHAYA

MWIMBAJI wa nyimbo za asili ya kabila la Kihaya, Saida Karoli amesema kuwa kwa sasa hawezi kuimba nyimbo zake kwa lugha hiyo ya Kihaya tu kwa madai kwamba mashabiki wake ni wa makabila mbalimbali.

“Sio makabila tu bali nina mashabiki kutoka mataifa mbalimbali pia, hivyo siwezi kuendelea kuimba kwa lugha yangu ya Kihaya, kwani kufanya hivyo ni kutaka kupoteza mashabiki,” alisema Saida.

Msanii huyo ambaye kwa sasa amejichimbia mkoani Mwanza akidai kwamba huko ndiko kwenye soko kubwa la muziki wake, alisema ingawa wimbo “Maria Salome” ndio uliomtoa lakini hivi sasa hana budi kuimba kwa kutumia vionjo tofauti.


Alisema, hata Diamond aliyeurudia wimbo huo hakauimba kwa Kihaya lakini umepokewa vizuri na kufafanua kuwa hiyo ni dalili tosha kwamba sio lazima aimbe kwa kutumia lugha hiyo.

No comments