VANESSA MDEE APATA SHAVU LA KUANDIKA WIMBO MPYA WA MAFIKIZOLO

NI muda wa kufurahia japo kwa kidogo tunachoendelea kukiona kinachotokea kwenye muziki wa Bongofleva kwa kupiga hatua baada ya Vanessa Mdee kupata shavu la kuandika wimbo mpya wa kundi la Mafikizolo kutoka afrika Kusini.

Wimbo huo ambao unatarajiwa kuachiwa hivi karibuni, umepewa jina la Kiswahili “Kucheza”, huku ukitayarishwa na Dj Maphorisa kutoka nchini humo.


Kupitia mtanda wa Instagram mmoja wa memba wa kundi hilo, Nhlanhla Nciza amefunguka hilo kwa kuandika akithibitisha.

No comments