VANESSA MDEE AZIDI KUPASUA ANGA NIGERIA

NYOTA wa kike wa Bongofleva nchini, Vanessa Mdee amezidi kupaa nchini Nigeria baada ya wimbo alioshirikishwa na nyota wa muziki nchini humo, Ice Prince wa "No Mind Dem" kuingia katika orodha mpya ya msanii huyo itakayotoka mwezi huu.

Ice Prince amemshirikisha Mdee katika wimbo huo ambao ameutaja kuwa kati ya nyimbo zitakazokuwa kwenye albamu yake mpya ya "Jos To The World."


Albamu hiyo mpya inatarajia kuingia sokoni Oktoba 28, mwaka huu na pia itakuwa inapatikana kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii.

No comments