Habari

WACHEZAJI CHELSEA WALIVYOAMUA KUMPIGANIA KOCHA WAO ANTONIO CONTE DHIDI YA LEICESTER

on

Defender David Luiz (No 30) looks delighted as he enjoys Moses' goal, which was assisted by Nathaniel Chalobah
WAKATI wacheza ‘kamari’ wakibashiri kutimuliwa kwa kocha wa Chelsea Antonio
Conte, wachezaji wa klabu hiyo wameamua kumpigania kwa kutandaza soka la hali
ya juu.
Katika juhudi hizo, wachezaji wake wakaangusha kipigo kizito cha 3-0
kwa mabingwa watetezi wa Premier League Leicester City.
Kwenye mchezo huo wa Ligi Kuu uliopigwa Jumamosi mchana, Chelsea
walitakata vilivyo huku kama kawaida yake Conte akihaha kwenye eneo lake la
kujidai, akitoa maelekezo kwa kila staili.
Costa, Eden Hazard na Victor Moses ndiyo waliopeleka kicheko Stamford Bridge
na kupunguza gumzo la ubashiri wa kutimuliwa kwa Conte.
Eden Hazard rounds Kasper Schmeichel to extend Chelsea's lead over Leicester City with a composed 32nd-minute goal
Eden Hazard akimchambua kama karanga kipa Kasper Schmeichel na kuifungia Chelsea bao la pili dakika ya 33
Premier League champions Leicester fell behind at Stamford Bridge after Diego Costa's seventh-minute opener
Diego Costa akiifungia Chelsea bao la kwanza dakika ya saba
Spain international striker Costa dedicated his goal to team-mate Willian's mother who passed away this past week
Hivi ndivyo Costa alivyoshangilia bao lake kwa kuonyesha ishara ya kuomboleza kifo cha mama mzazi wa mchezaji mwenzake  Willian kilichotokea wiki hii
Nigeria international winger Moses continued his fine form this season with a well-taken strike in the 80th minute
 Moses anaendelea kung’ara msimu huu
Moses akishangilia kwa staili ya sarakasi baada ya kuipa Chelsea bao la tatu dakika ya 80

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *