Habari

WACHEZAJI WABAGUZI KUFANYA MAZOEZI NA WANAWAKE

on

WACHEZAJI wawili wa timu ya
soka ya Sparta Prague wameambiwa kufanya mazoezi na timu ya wanawake baada ya
kutoa matamshi ya kiubaguzi dhidi ya maafisa wanawake wanaosimamia mechi.
Kipa Tomas Koubek mwenye umri
wa miaka 24, alisema kuwa: “Wanawake wanafaa kuwa jikoni baada ya naibu refa
Lucie Ratajova kushindwa kuinua bendera kwa mchezaji ambaye alikuwa ameotea
wakati wa mechi ya siku ya Jumapili ambapo walitoka sare ya 3-3 na Brno.
Kiungo wa kati, Lucas Vacha
mwenye umri wa miaka 27 alichapisha picha katika mtandao wake wa Twitter ikiwa
na matamshi: “Waelekee jikoni.”
Ofisa mkuu wa klabu ya Sparta,
Adam Kotalik aliyataja matamshi hayo kama yasiyokubalika.
akizungumza baada ya mechi ya
Jumapili, raia huyo wa Jamhuri ya Czech aliongezea: “Wanawake hawafai kusimamia
mechi za wanaume.”

Baadae alichapisha picha ya
mkwe na mwanawe wa kike katika mtandao wa facebook na kusema “Ningependa kuomba
msamaha kwa wanawake wote.”

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *