WASAMBAZAJI FILAMU INDIA WAFANYA MGOMO BARIDI "KUWAKATAA" WAPAKISTAN

WASAMBAZAJI wa kazi za sanaa nchini India wameamua kutozingiza sokoni filamu zote za wasanii wa Bollywood ambazo zimewashirikisha wasanii kutoka nchini Pakistan.

Uamuzi huo uliofikiwa na Indian Motion Pistures Producers Association (IMPPA), umeshutumiwa vikali na wasanii kutoka jimbo la Kashmir, Pakistan kwani utawafanya wayumbe kiuchumi.

Katika taarifa yao, wasanii hao wamesema masuala ya kisiasa hayapaswi kuingizwa kwenye kazi kwa kuwa wanaoathirika sio wanasiasa bali wasanii.


Mmoja wa wasanii hao, Kamal Hyder, alisema kibaya zaidi ni kwamba filamu zao zimepigwa marufuku kuonyeshwa katika kumbi za burudani na vituo vya televisheni nchini India.

No comments