WEMA SEPETU AWATAKA "WAVIMBA MACHO" WAMWACHE AUNTY EZEKIEL

WEMA Isaac Sepetu “Madam” amefunguka kuwa anachukizwa na watu wanaomtelea matusi mwigizaji mwenzake Aunti Ezekiel baada ya kuhudhuria sherehe ya kuzaliwa ya mzazi mwenza wa Nasib Abdul, Zarinah Hassan "Zari The Boss Lady."

Akizungumza, Wema alisema unatakiwa ufike wakati watu waelewe na waongozwe kwa akili zao za kuzaliwa kwa sababu hakuna kitu kibaya ambacho amekifanya Aunty kwa kuwa staa mwenzake huyo kwa sasa ni mmoja wa familia hiyo.


“Jamani hebu naomba kwanza wamuache Aunty, hana kosa lolote, hata kama ningekuwa mimi hapa nisingeweza kuacha kwenda kwa sababu tayari ni familia na hawezi kumuacha mumewe aende peke yake maana vitu vingine ni vya kujiongeza tu, nachukizwa sana na jinsi wanavyomrushia maneno ya kashfa,” alisema Wema.

No comments