WEMA SEPETU: JAMANI MSINIZUSHIE MAMBO YASIYOFAA SASA MIMI NI MTU MZIMA

MREMBO na msanii nyota wa Bongo Movies, Wema Sepetu amesema kwa sasa yeye ni mtu mzima ambaye anaweza kukaa na kutoa ushauri utakaoisaidia jamii inagawa baadhi ya watu wasiopenda maendeleo yake humzushia amefanya matukio mbalimbali yasiyofaa.

“Mimi sio malaika bali binadamu kama wengine ambaye ninaweza kufanya makosa lakini ajabu ni kuwa nikifanya kosa la kibinadamu ninaandamwa sana. Ukweli unabaki palepale kwamba nimekuwa mtu mzima ninayeweza kutoa ushauri,” alisema Wema.

Alisema kuwa binadamu anapitia hatua mbalimbali za makuzi na hawezi kuendelea kufanya mambo ya kitoto wakati tayari ni mtu mzima huku akiwataka wale wanaomsakama kulitambua.


“Ukifuatilia utagundua kuwa hata lile kundi lililokuwa linajiita “Team Wema” nilikataa kwa sababu lililenga kunichafulia mbele ya jamii ili nionekane ninaruhusu mambo yasiyo na manufaa kwa umma,” alisema mrembo huyo wa Tanzania mwaka 2006.

No comments