WENGER ASEMA SIO LAZIMA ABEBE TAJI LINGINE KABLA HAJAAGA ARSENAL

KOCHA Arsene Wenger amesisitiza kuwa sio lazima abebe taji lingine England kabla hajaondoka Arsenal.

Wenger raia wa Ufaransa juzi ametimiza miaka 20 ya kufundisha klabu hiyo ya Kaskazini mwa Jiji la London lakini kwa miaka ya karibuni amekuwa kwenye maumivu ya kushidwa kutwaa taji kama ilivyokuwa awali.

Tangu mwaka 2005 Gunners wameshinda mataji mawili tu ya FA tofauti na miaka saba nyuma waliyoitumia kutwaa mataji saba makubwa.

Alipoulizwa kama ana dhamira ya kutwaa taji kabla ya kuondoka, Wenger (66), alisema: “Jambo moja muhimu mashabiki bado wanahitaji niendelee kubaki." 

"Kinachonifanya nitamani kuendelea kubaki ni kwamba najiona kama kuna mambo mazuri naweza kuendelea kufanya kwenye klabu.”

No comments