WENGER AWATAKA WACHEZAJI WAKE KUZIDI KUKAZA

KOCHA Arsene Wenger amewataka Arsenal kuendelea kukaza buti zaidi baada ya kuonyesha kiwango cha hali ya juu katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Ludogorets.

Katika mchezo huo uliopigwa kwenye uwanja wa Emirates, Gunners waliibuka na ushindi wa mabao 6-0, huku straika wao, Mesut Ozil akitupia “hart trick” na kuwapa ushindi huo mnono uliowafanya kukaa kileleni mwa Kundi A.

Kutokana na kiwango hicho, Wenger anajivunia na timu hiyo lakini bado hajaridhika zaidi kutokana na kuwa bado ni hatua ya mwanzo ya michuano hiyo.

“Mambo yanaweza kuwa magumu, sio vizuri kuanza kuridhika,” alisema kocha huyo.

“Tumefunga mabao mengi na kuendelea kubaki bila kufungwa. Tulikuwa wepesi na tishio, tulijiambia ni lazima tuendelee kuwa hivyo kwa kila mechi ila Ludogorets walicheza vizuri kipindi cha kwanza,” aliongeza kocha huyo.


Kutokana na matokeo hayo, Arsenal inaweza kutinga hatua ya 16 endapo wataifunga Ludogorets nchini Bulgaria, lakini imeshawahi kutupwa nje ya michuano hiyo katika hatua hiyo misimu ya nyuma.

No comments