WERDER BREMEN YADAI "HAKUNA SHIDA" KUMPOTEZA SERGE GNABRY

TIMU ya Werder Bremen imesema kwamba haihofii kumpoteza kinda wake, Serge Gnabry kutokana na kuonyesha  makali mwanzoni mwa maisha yake kwenye klabu hiyo ya Weserstadion.

Gnabry alionyesha kandanda safi akiwa na kikosi cha Ujerumani kilichoshiriki kwenye michuano ya Olimpiki ya Rio ikiwa ni baada ya kuondoka Arsenal kabla ya msimu huu kuanza baada ya kukosa nafasi ya kucheza kwenye klabu hiyo ya Emirates.

Tangu kinda huyo mwenye umri wa miaka 21 atinge kwenye klabu hiyo, Frank Baumann amesema kuwa Gnabry hatakwenda mahali popote.


“Serge anadai alifanya uamuzi wa kuondoka kwenye klabu kubwa ili aweze kupata mahali ambapo atapata nafasi ya kucheza mara kwa mara,” mkurugenzi huyo aliliambia gazeti la Bild.

No comments