Habari

WEWE NI MWANAMUZIKI WA DANSI? CHANGAMKIA FURSA HII KUTOKA CHOICE FM

on

KIPINDI cha Choice Bambataa cha kituo cha radio cha Choice FM cha
jijini Dar es Salaam, kinakuja na mkakati mzuri wa kuunyanyua muziki wa dansi.
Choice Bambataa kimesema moja ya hatua zao za kuusukuma mbele muziki
wa dansi, ni kusaidia kuwaingiza studio wanamuziki wa dansi  na kurekodi nyimbo zao bure na kisha
kufanyiwa promosheni ya hali ya juu kupitia kipindi hicho kinachoruka kila siku
za Jumatatu hadi Ijumaa.
Akiongea na Saluti5 mmoja wa watangazaji wa kipindi hicho cha Choice
Bambataa, Irine Gabriel (pichani juu), alisema hawaangalii ukubwa wa jina la mwanamuziki,
bali watakachoangalia ni uwezo na ubora wa kazi za msanii kulingana na soko la
sasa.
“Lengo la kipindi chetu katika mpango huu, ni kuwasaidia wanamuziki wa
dansi ambao wana kazi nzuri lakini hawana uwezo wa kuingia kwenye studio za
kisasa na kurekodi nyimbo zao,” anaeleza Irine.
“Tutagharamia kuwaingiza studio na kuhakikisha wanaibuka na kazi zenye
kiwango cha hali ya juu,” aliongeza mtangazaji huyo wa Choice Bambataa.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *