WILSHERE AANZA KUMKUNA BOSI WA BOURNEMOUTH

MWENYEKITI wa klabu ya Bournemouth, Jeff Mostyn ameonyesha kupendezwa na huduma ya kiungo kutoka Uingereza na klabu ya Arsenal, Jack Wilshere aliyesajiliwa kwa mkopo mwishoni mwa mwezi uliopita.

Mostyn amesema tangu kiungo huyo alipojiunga na klabu ya Bournemouth, kikosi chao kimekuwa na mabadiliko maubwa katika safu ya kiungo na anaamini endapo watawasilisha maombi ya kumsajili moja kwa moja, hakuna litakaloshindikana.

Wilshere tayari ameshaitumikia Bournemouth katika michezo mitatu ya Ligi Kuu Uingereza na amekuwa mmoja wa watu wanaovutiwa na kiwango chake kila kukicha.

“Tunaweza kufanya hivyo. Naamini hakuna litakaloshindikana kwasababu wilshere anahitaji kucheza kila juma kama ilivyo hivi sasa.”

“Huenda ikawa wakati wa usajili wa mwezi Januari ama mwishoni mwa msimu huu. Tutajaribu kufanya hivyo na naamini tutafanikiwa. Niwe muwazi, kiwango cha Wilshere ni kikubwa na kinaonyesha kuisaidia klabu yetu,” alisema Jeff Mostyn.


Hata hivyo mpango uo wa Jef Mostyn huenda ukapingwa vikali na meneja wa arsenal, Arsene Wenger ambaye anaamini umpeleka Wilshere kwa mkopo katika klabu ya Bournemouth ilikuwa ni moja ya hatua ya kuta kulinda kipaji chake kwa ajili ya maisha yake ya baadae ndani ya washika mtutu wa kaskazini mwa jiji la London.   

No comments