ZINEDINE ZIDANE AENDELEA KUGOMA KUMTOA JAMES RODRIGUEZ

WAKATI ambapo James Rodriguez anahusishwa na tetesi za kutaka kutua kwa mashetani wekundu wa jiji la Manchester, klabu yake ya Real Madrid imekataa ofa yoyote.

Rodriguez mwenye umri wa miaka 25 amekuwa na mafanikio makubwa tangu atue mwaka 2014 katika kikosi cha Los Blancos.

Akinukuliwa juu ya kumkatalia kuondoka, kocha Zinedine Zidane aliema: “Rodriguez ni mchezaji muhimu ndani ya Real Madrid.”

“Tetesi za sasa ni za kupuuzwa kwani Real Madrid haina mpango wa kuachana na straika huyu.”

“Tunatambua kwamba Manchester United na Chelsea wamo mbioni kutaka saini yake lakini nimekaa na Rodriguez na kukubaliana baadhi ya mambo.”


“Nimemwakikishia nafasi katika kikosi cha kwanza , nimemwambia bado ninaendelea kumwamini.”

No comments