ZLATAN IBRAHIMOVIC KUTUA DELH DYANMOS BAADA YA MANCHESTER UNITED

KOCHA wa timu ya Delh Dyanmos, Gianluca Zambrotta amesema kwamba ana mpango wa kumsajili straika Zlatan Ibrahimovic kutoka Manchester United pindi mkataba wake utakapomalizika.

Ibrahimovic alijiunga na Manchester United akitokea Paris Saint-Germain kabla ya msimu huu kuanza na amekuwa na mwanzo mzuri kwenye klabu hiyo ya Old Trafford kwa kufunga mabao manne katika mechi saba za Ligi alizocheza.

Staa huyo mwenye umri wa miaka 35, mkataba wake na mashetani hao wekundu unatarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu huu na Zambrotta ameshatangaza kuhakikisha anampeleka nchini India.

“Kutokana na kuwa ana mashabiki wengi India nadhani Zlatan atapenda kumaliza kibarua chake hapa nchini,” Zambrotta aliliambia gazeti la Indian Exepress.


“Kwangu mimi ninajaribu kumshawishi ili aweze kuichezea timu ya Delhi Dynamos,” aliongeza kabla ya kusema kuwa hivi karibu India itakuwa ni sehemu nzuri kwa wanasoka wa kimataifa.

No comments