ALEX FERGUSON AMPA CRISTIANO RONALDO TUZO YA BALLON D'OR

KOCHA mkogwe aliyemwaga mafanikio yasiyopimika uwanja wa Old Trafford, Alex Ferguson amesema tashangaa kama tuzo ya Ballon d’Or haitatua mikononi mwa nyota wa zamani wa Manchester United Ctistiano Ronldo.

Fergusoni ndiye aliyeisaidia kwa kiasi kikubwa mafanikio ya Ureno alipomsajili akiwa na miaka 17 na kutengeneza kipaji chake kinachompa ulaji mkubwa hivi sasa.

“Sioni yeyote anayeweza kuchukua tuzo ya Ballon d’Or zaidi ya Ronaldo,” alisema Ferguson wakati akizungumza na MARCA.


“Mafanikio yake hayawezi kusambaratishwa na mchezaji yeyote, amekuwa na mwaka mzuri Barcelona na timu ya taifa Ureno pamoja na kushindwa kumaliza mechi ya fainali ya Euro 2016 kutokana na kuumia.

No comments